Monday, April 27, 2009

KWANI WAO WAWEZE WANA NINI HATA MIMI NISHINDWE NINA NINI???




Hayo sio maneno yangu ndugu wadau ni maneno ya Bibi Bette Calman kutoka nchini Australia mwenye umri wa miaka 83 ameuonyesha ulimwengu kuwa hata kama ana umri mkubwa unaweza kuumudu mwili wake.. Bibi huyu anayejipenda kimavazi huwaacha watu midomo wazi kwa uwezo wake wa kupiga push ups na kujipindapinda uwezo pamoja na kuwa na umri huo ambao wazee wengi wa umri wake hawawezi na hulalamikia maumivu ya viungo vyao kwa kisingizio cha umri . Bibi huyu ni mwalimu wa yoga na anayoyafanya hata baadhi ya vijana wengi hatuwezi kuyafanya..pengine hata wewe unayeisoma habari hii huwezi kufanya nadanganya??
Kama unabisha naomba upige push ups ishirini tuone utakavyo kosa kupumua kwa amani, Jamani vijana wenzangu mazoezi ni muhimu sana.

No comments: