Sunday, October 25, 2009

Mambo Ya Kuchukua Waume Na Wake za Watu





Ukiwa unapenda raha usisahau kuna karaha pia ndani yake, sasa kama umezoea vya wizi jua ipo siku itakukuta hii kama ambao wana ndoa hawa walivyokosa adabu sasa ona mambo waliyoyapata

MARUBANI WASAHAU KUTUA NDEGE


Wasiwasi mkubwa uliwakumba wana anga wa kimarekani siku ya ijumaa tarehe 23 october pale ambapo ndege ya NWA ilipokosa mawasiliano kwa kipindi cha dakika 78. Ndege hiyo ambayo ilikuwa inatokea San Diego kuelekea Minneapolis na ikiwa imebeba abiria 144.
Pamoja na jitihada za kuwapigia simu na kufanya mawasiliano ya aina yote bila mafanikio iliwafanya Wana Anga wakimarekani kupeleka mawazo yao moja kwa moja kuwa ndege hiyo imetekwa nyara.

"Tulikuwa tukiwaona kwenye radar na kuwazungumzisha ila hatukupata jibu, hilo jambo lilitutia wasiwasi sana hayo" ni maneno ya msemaji mkuu wa wana anga hao mr Toni Molinari.
Imesadikiwa ya kuwa marubani hao walipitiwa na usingizi ndio maana hawakuweza sikia wala kujibu ujumbe wowote uliotumwa kwao.

Thursday, October 22, 2009

WAPENDA VIATU MPOOO? SPECIAL KWA KINA DADA









/>


Hayaa hayaa hayaa shughuli imeingia mvua masheikh wanakula wima. masistadoo si huwa mnadai mnapenda sanaa hills, hivi ni viatu vya pekee hivi mtu ukivaa utajiskiaje???

WAKATI WA SODOMA UMEWADIA





Hii ndo hali ya dunia yetu kwa sasa, matendo ya ajabu na yanazidi kuongezeka, kama unavyoona pichani hapo juu.
Daniel Chege Gichia (kushoto, mwenye ndevu) ambaye ni bibi harusi akiwa na bwana harusi wake Charles Ngengi wakati wa ndoa yao.

Ndoa iliyofungwa hivi karibuni jijini London, Uingereza, kati ya wanaume wawili, raia wa Kenya, Daniel Chege Gichia (mwenye umri wa miaka 39) na Charles Ngengi (40), imezua gumzo kubwa miongoni mwa wananchi nchini Kenya... hali hii inaongezeka sana
kwa kasi sijui tutafika wapi.

Na picha ya chini ni kati ya wanandoa wawili kutoka nchini marekani Bwana Jamil na Bi Michael. oops na Michael aliyeshika maua, ambao pia waliingia katika ulimwengu huu wa sodoma week chache zilizopita. Mungu atuepusha kua miongoni mwao ni kinyume cha mila na desturi zetu.