Saturday, September 19, 2009

EID MUBARAK



Asalaam aleykum warahma tullah taala wabarakat. kwa niaba ya waislam wenzangu ningependa kuwatakia waislam wote duniani Eid njema. Tunaomba Mwenyezi Mungu azikubali funga zetu na sala zetu na atujaalie tuweze kufunga ramadhani zifuatazo. Inshallah

Tuesday, September 15, 2009

MRUSHA VIATU MAARUFU DUNIANI AACHIWA HURU



Mwandishi wa habari ambae alimrushia kiatu rais wa zamani wa marekani bwana G.Bush ameachiwa huru leo, mwandishi huyu ambae anajulikana kwa jina la Muntazer Al Zaid amejipatia umaarufu kwa kitendo chake kinachoitwa cha ushujaa kwa kumrushia rais mstaafu huyo viatu, kwa kile alichosema ni msisitizo wa kutaka wanajeshi wa kimarekani waondoke nchini irak.
Aliachiwa huru tangu jana ila kutokana na kutotimia kwa baadhi ya fomu za kuachiwa huru ikabidi atoke leo, Anasema kuwa alipata mateso mengi sana moja wapo ni kupigwa shoti ya umeme nk. ila anafuraha kwa kuwa huru, na watu wanamuona ni shujaa.

Monday, September 14, 2009

MPAKANJIA AFARIKI DUNIA


Habari zilizotufikia hivi sasa zinasema kuwa MOHAMED MPAKANJIA amefariki dunia! Akithibitisha kifo hicho, jamaa wa karibu wa mfanyabiashara huyo, alisema kuwa Medy amefariki leo mchana katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam alikopelekwa jana usiku akitokea kwa Dk Massawe wa Temeke, ambako alikimbizwa kwa huduma ya kwanza. Habari zinasema kuwa Medy, ambaye alikuwa mume wa marehemu Amina Chifupa, hali yake kiafya haikuwa nzuri katika siku za hivi karibuni. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI - AMIN!!!!