Hayo sio maneno yangu ndugu wadau ni maneno ya Bibi Bette Calman kutoka nchini Australia mwenye umri wa miaka 83 ameuonyesha ulimwengu kuwa hata kama ana umri mkubwa unaweza kuumudu mwili wake.. Bibi huyu anayejipenda kimavazi huwaacha watu midomo wazi kwa uwezo wake wa kupiga push ups na kujipindapinda uwezo pamoja na kuwa na umri huo ambao wazee wengi wa umri wake hawawezi na hulalamikia maumivu ya viungo vyao kwa kisingizio cha umri . Bibi huyu ni mwalimu wa yoga na anayoyafanya hata baadhi ya vijana wengi hatuwezi kuyafanya..pengine hata wewe unayeisoma habari hii huwezi kufanya nadanganya??
Kama unabisha naomba upige push ups ishirini tuone utakavyo kosa kupumua kwa amani, Jamani vijana wenzangu mazoezi ni muhimu sana.
Haya ndugu wapendwa mambo ndo hayo kwa wale wanaopenda kujirusha, Kituo kipya cha maraha cha Savannah Lounge & Bar kimefunguliwa rasmi leo katika hotel ya Paradise City ambayo ipo katika jengo la Benjamin Mkapa Tower mtaa wa Azikiwe Avenue opposite na posta mpya. kazi kwenu wadau
Hawa ni wadada wa Tanzania waishio mjini DC Washington, wakiwa katika swala zima la kukonga nyoyo zao, katika style ya kipekee ile ipendwayo na watu wengi kabisa ya pinda mugongo, haya sasa jamani kazi ipo hapo,
Sheikh yahya hussein anasema bado yuko hai na anaendela vizuri tuu, hayo aliyasema akiwa nyumbani kwake mara tuu alipoongea na waandishi wetu wa habari, pembeni yake ni mkewe bi fetty,
Hii ndio ramani mpya ya jiji la dar es salaam tanzania, ambayo inatarajiwa kuanzwa kushugulikiwa haraka iwezekanavyo baada ya pesa za epa kurejeshwa zote, Imekuwa ni ndoto ya kila mtanzania kutaka kuona mji mpya wa dar es salaam ukijengwa upya na kuwa wa kisasa kama ramani yake inavyoonekana juu pichani,
Katika hali isiyo tegemewa nchini italy yametokea maafa makubwa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 270, watu wengine zaidi ya kumi elfu kukosa mahali pa kushi na zaidi ya 1500 wakiwa majeruhi, tukio hilo lilitokea alfajiri ya mapema ya jumanne tarehe 7 april huko mjini L'Aquila.
Mashabiki wa muziki wa taarabu wakiwa wamepandisha mzuka hapa hawaambiwi wala hawasikii labda mpaka kinanda kizimwe, kama wenyewe wasemavyo mdadi wa mcheza taarabu wakuutuliza mpiga Kinanda
Mwanadada huyu pichani (kulia) akikata nyonga si kawaida huku akina kaka ambao mara nyingi hutokwa na udenda, wanapoona nyonga za akina dada zikikatwa, wakijifanya kuwa biiize kama kuna kitu kingine wamefuata tofauti na nyonga za akina dada hao
Wakati wote ukumbini hapo midume ndio iliyokuwa ikionekana kukata nyonga, kama inavyoonekana pichani wakati muimbaji wa kundi hilo mwanadada, Isha Makongo 'Mashauzi' aliyesimama (katikati) akiimba. Siku hizi kwenye taarabu, wanawake ndio wamekuwa watazamaji wa nyonga za akina kaka zikifanya kazi.
Kundi la Jahazi Modern Taarabu, usiku wa kuamkia leo lilifanya makamuzi 'ya kufa mtu' katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa kundi hilo Mzee Yusuph, akiwapelekesha puta mashabiki wa kundi hilo (hawapo pichani) kwa kibao cha VIP.
Bendi ya muziki wa dansi ya Diamond Muzika usiku wa kuamkia leo ilifanya vitu vyake katika Ukumbi wa Mango Garden, ulipo Kinondoni Jijini Dar es Salaam, kama anavyoonekana pichani muimbaji wa bendi hiyo Hassan River (katikati) akilishambulia jukwaa pamoja na wanenguaji wa bendi hiyo.
pichani mama salma kikwete , mke wa Rais wa awamu ya nne ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, mama Salma kikwete akisaidia kumsukumia mkazi wa Dar es salaam kiti bi Rehema nditi ambaye ana matatizo ya mguu na mkono, pembeni yao anayetazama ni mtoto pekee wa bi nditi mwenye miaka 24 anayeitwa maliki, mungu ashukuliwe
Huwezi amini katika maisha ya mtanzania bado ni kitendawili katika swala zima la sekta ya miundombinu, siku mvua inaponyesha basi inakuwa ni kama kiyama kwa mtanzania , bara bara zinafurika , foleni haziishi, na hata maji taka hayana pa kwenda, je lini tutafika jamani namna hii.
Mheshimiwa kikwete akiwa na baadhi ya wazee wenzake wanaotawala naye nchi , Seif shariff hamad pamoja na mheshimiwa Abraham lipumba, mala baada ya kutokea katikahoteli ya lamada jijini Dar es salaam ilipokuwa ikifanyika ibada ya dua ya kumuombea Shekhe Shaaban khamis Mloo