Saturday, June 20, 2009

WATANZANIA WAISHIO MJINI ATHENS NCHINI GREECE WAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI


Kiutendaji, jumuiya hii ilikuwa ikiendelezwa na watu wachache waliokuwa na moyo na upendo wa kuona umoja wa watanzania unaendelea na kudumu. Watu hao baada ya kugundua kwamba muda muwafaka wa kufanya uchaguzi umewadia, na kwamba watu wanahitaji mabadiliko, walikubaliana kwa pamoja zitafutwe mbinu zitazohakikisha ufanikishaji wa uchaguzi.


Na hapo ndipo zilipoanza kampeni za uchaguzi, ambao ulifanyika katika ukumbi wa Sieraleone siku ya Jumamosi 07/03/2009 kuanzia saa moja usiku hadi saa tisa.Ulikuwa ni uchaguzi ULIOFANA na wa HAKI. Takriban watanzania wote walihudhuria, hata wale ambao siku za nyuma walikuwa hawana hamasa kabisa na jumuiya.Kulikuwa na kila aina ya viburudisho, vilivyosindikizwa na na mziki wa kupendeza .

Katika uchaguzi huu walichaguliwa viongozi wapya wafuatao:


MWENYEKITI
ABDALLA MOHAMED ALI. (AMASHA)

MAKAMU M/KITI
SALUM FRANCIS WILLIAM. (Mzee FRANCIS.)

KATIBU MKUU
KAYU ALLY LIGOPORA. (KAYU)

KATIBU MSAIDIZI
MUNGI HUSSEIN SALUM. ( MUNGI)
MWEKA HAZINA
AZIZI ALI. ( AZIZI )

NAIBU MWEKA HAZINA
CHINA SELEMAN HASSAN. (CHINA)

AFISA WA JAMII
ALLY MOHAMMED UBAO. ( ALI UBAO)


WAJUMBE WA KAMATI :
1 ALLY SALUM NYAU. ( ALI NYAU )
2 MWANSITI ISSA MNTAMBO. ( MWASITI )
3. MWAMVITA HATIBU MAKENGA ( MACHO )

No comments: