Saturday, June 20, 2009

SHIRIKA LA AL LAONYA KUWA MATESO BADO YAPO ZIMBAMWE


Shirika la Kutetea Haki za binadamu Amnesty International limeilaumu serikali ya Zimbabwe kwa kuendelea kuhusika na vitendo vya mateso yanayokiuka haki za binadamu.Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Shirika hilo Irene Khan aliyefanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara ya siku 6 nchini Zimbabwe.

Kulingana na Bibi Khan visa vya ghasia zilizo na misingi ya kisiasa vimepungua ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita lakini bado vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinaendelea kutokea.Kauli hizo zimetolewa wakati ambapo wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na Zimbabwe wamefanya mazungumzo rasmi ya kwanza katika kipindi cha miaka 7 iliyopita.Kamishna wa masuala ya misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Ulaya Louis Michel aliyezungumza na waandishi wa habari mjini Brussels baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai alisema kuwa Umoja huo una azma ya kurejesha uhusiano kati yao baada ya kutatua baadhi ya masuala yanayozua mitazamo tofauti.

No comments: