Thursday, June 11, 2009

TRUE LOVE EXIST





NI NDOA YA UKWELI KATI YA WAIGIZAJI WA FILAMU ZA KIBONGO AMBAPO WANAFILAMU YAO YA MBONI YANGU (SAJUKI NA WASTARA).....WALIYOIGIZA KABLA YA KUPATA AJALI ILIYOPELEKEA WASTARA KUKATWA MGUU.....HAKIKA HII INAPENDEZA NA INAONESHA UPENDO WA KWELI "UPENDO WA UJASIRI"...HONGERENI WASTARA NA SAJUKI
sherehe hiyo ilitawaliwa na vilio na majonzi, hasa pale Bibi harusi alipoingia kwenye eneo la wazi lililoandaliwa kwa shughuli hiyo akiwa amekaa kwenye baiskeli ya gurudumu (Wheel Chair).
Mke wangu sitakuacha, wewe ni mahabuba wangu, sitakuacha,” Sajuki aliimba wimbo huo. “Mume wangu unilinde, unipende, usiniache…,” Wastara naye alijibu na kusababisha vilio kutoka kwa wageni waalikwa. Aidha, yeye mwenyewe alishindwa kuendelea kuuimba wimbo huo na kujikuta akilia kwa uchungu mkubwa.
“Nimesimama hapa kwa ajili ya kumhakikishia nyonga mkalia ini wangu (Wastara) kuwa mimi ni wake milele sitomuacha mpaka kifo,” alisikika Sajuki.
Baada ya Shamrashamra hizo, Sajuki alimbeba Wastara huku akicheza naye wimbo wa mwanamuziki wa Sauzi, Yvonne Machaka ‘Chakachaka’ uitwao ‘Mkomboti’ huku akielekea naye kwenye gari kwa ajili ya kuondoka. Tukio hilo lilisindikizwa na wasanii kibao kwa nyuma huku wakicheza mpaka maharusi hao walipopanda gari na kwenda kwenye Fungate lao Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

No comments: