Thursday, June 25, 2009

MICHAEL JACKSON AFARIKI DUNIA


.

Michael suffered a cardiac arrest earlier this afternoon at his Holmby Hills home and paramedics were unable to revive him. We're told when paramedics arrived Jackson had no pulse and they never got a pulse back.

A source tells us Jackson was dead when paramedics arrived.

Once at the hospital, the staff tried to resuscitate him but he was completely unresponsive.

We're told one of the staff members at Jackson's home called 911.

La Toya ran in the hospital sobbing after Jackson was pronounced dead.

Michael is survived by three children: Michael Joseph Jackson, Jr., Paris Michael Katherine Jackson and Prince "Blanket" Michael Jackson II.

Tuesday, June 23, 2009

BALAA NDANI YA DC





Treni ya abilia imesababisha mauaji mjini dc washington, Treni hiyo inayojulikana kama metro ambayo huwa katika msitari mwekundu na inayofanya safari yake ya kusaidia usafiri kati ka miji ya dc , maryland na virginia, imesababisha mauaji yanayokusudia watu zaidi ya kumi kufa papo hapo na wengine zaidi ya 50 wakiwa majeruhi

Saturday, June 20, 2009

WAMAREKANI KUFUNDISHWA KIINGEREZA ASILIA TOKA AFRIKA


Afisa Mwandamizi wa ubalozi wa Marekani nchini Dr.Tulinabo Mushingi(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa vyuo vikuu wanaosomea shahada za kwanza wanaosafiri kesho kwenda Marekani kwa programu ya kufundisha lugha ya kiingereza kwa mataifa ya Afrika. Programu hiyo inagharimiwa na watu wa Marekani,ni programu inayofuzwa kwa kina inayolenga kuongeza usomaji kwa lugha ya kingereza,kuandika,kusoma na kusikiliza maarifa ya wanazuoni wa kiafrika lakini kubwa zaidi ni kuwapa uelewa mpana zaidi wa tamaduni za kimarekani pamoja na mila na desturi zao.

KUMEKUCHA TANZANIA MAMBO YA UCHAGUZI


Mgombea wa CCM Oscar Rwegasira Mukasa akijinadi wa wapiga kura katika Kijiji cha Mavota wilaya Biharamulo katika moja ya mikutano ya CCM ya kampeni kuwania kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi.Picha na Frederick Katulanda

RUBANI AFARIKI NDEGE IKIWA ANGANI, WATU WAOMBA SALA ZAO ZA MWISHO


Katika kisa ambacho wengi watadhani ni muujiza, abiria 247 waliokuwa wakisafiri na ndege ya kampuni ya Continental kutoka Ubelgiji hadi Marekani waliponea chupuchupu wakati nahodha wa ndege yao alipofariki dunia.
Msemaji wa Halmashauri inayosimamia usafiri wa ndege Marekani, Arlene Salac alisema kulikuwa na marubani wengine wawili ambao waliidhibiti ndege hiyo aina ya Boeing 777 hadi uwanja wa ndege wa Newark Liberty ambako ilitua kwa dharura.

Mtaalamu mmoja wa usafiri wa ndege, Jim Ferguson alisema si jambo la kawaida rubani kufariki dunia akiwa angani.

Kwa kawaida ndege hiyo huendeshwa na marubani wawili. Lakini kwa bahati nzuri wakati huu, kulikuwa na mwingine wa ziada.

Bwana Ferguson alisema ingekuwa vigumu kwa rubani mmoja kuidhibiti ndege hiyo kutua.

Abiria hawakuambiwa lolote kuhusu mkasa huo. Miongoni mwao alikuwa daktari mmoja wa maswala ya moyo, Dr. Julien Struyven ambaye aliitikia tangazo daktari yeyote kwenye ndege hiyo kujitokeza.

Abiria hawakujua kwamba mwito ulitolewa kwa ajili ya kumuokoa rubani wa ndege hiyo.

Dr Struyven alipomfikia rubani huyo alikuta kama tayari ameaga dunia.

“Hakukuwa na uwezekano wowote wa kumwokoa,” alisema Dr Struyven.

Alisema huenda rubani huyo mwenye umri wa miaka 60 na ambaye amehudumia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20 alifariki dunia kutokana na matatizo ya moyo

WAZIRI WA ULINZI NCHINI SOMALIA AUWAWA


Waziri wa usalama wa ndani wa Somalia Omar Hashi Aden ameuwawa kwenye shambulio la kujitoa muhanga la bomu lililotegwa kwenye gari kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.
Watu wengine zaidi ya 20 wameuwawa kwenye mlipuko huo katika Hoteli ya Beledweyne, kaskazini mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Miongoni mwa waliouwawa ni maafisa kadhaa wa Kidiplomasia wa Somalia.

Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed amelaumu kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabaab , ambalo pia baadaye lilikiri kufanya shambulio hilo.

Kundi hilo linaaminika kuwa na uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al -Qaeda.

Siku ya jumaatano watu 10 walikufa wakati kombora liliporushwa kwenye msikiti mjini Mogadishu.

Katika shambulizi la Alhamisi , walioshuhudia walisema mlipuaji wa kujitoa muhanga alilipua gari lililojaa mabomu kwenye hoteli ya Medina , mjini Beledweyne, yapata Kilomita 400 kaskazini mwa Mogadishu.

Abdulkarim Ibrahim Lakanyo, balozi wa zamani wa Somalia nchini Ethiopia pia ameripotiwa kuwa miongoni mwa waliouwawa.

Mwandishi wa BBC Will Ross anasema bwana Aden alihamia mjini Beledweyne hivi majuzi, mji ulioko karibu na mpaka wa Ethiopia, katika jitihada za kukomesha wanamgambo wa Kiislamu wasiendelee kuthibiti maeneo mengi zaidi.

Rais Ahmed ameambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Mogadishu kwamba Somalia imevamiwa na magaidi wasiotaka kuona benderea ya nchi hiyo, wala amani .

Amesema kundi hilo la Al- shabaab linajificha kwenye Uislamu kuendesha ukatili wao.

Somalia haijawa na serikali dhabiti tangu mwaka wa 1991 , na zaidi ya watu milioni nne , ambao ni asilimia 75 ya raia wa nchi hiyo wanahitaji msaada wa chakula.

Kundi la Al- Shabaab ni mshirika katika muungano wa wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali ambao wamekuwa wakijaribu kuiangusha serikali ya mpito ya Somalia inayoungwa mkono na umoja wa mataifa.

Rais Ahmed , ambaye mwenyewe ni muislamu mwenye msimamo wa wastani alichukua khatamu nchini Somalia mwezi Januari , lakini hata baada ya kuanzisha utawala wa kuzingatia sheria za kiislamu , hatua hiyo bado haijawaridhisha wapiganaji hao.

Jumaatano , kamanda mkuu wa Polisi mjini Mogadishu aliuwawa kwenye mashambulizi dhidi ya ngome za wanamgambo.

Mwakilishi wa shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR nchini Somalia amesema umwagikaji damu wa hivi karibuni nchini Somalia ndio mbaya zaidi kuikumba nchi hiyo kwa muda wa karibu miaka 20.

OBAMA KUFANYA MABADILIKO YA UCHUMI NCHINI MAREKANI


Mfumo huu mpya unalenga kuilinda Marekani kukumbwa na mzozo wa kuichumi sawa na ulio sasa katika siku za usoni.

Rais wa marekani Barack Obama amependekeza kuufanyia mabadiliko makubwa mfumo wa uchumi wa marekani pamoja na njia ambazo zinaweza kuzuia mzozo mbaya wa kiuchumi kama ule uliopo sasa duniani kujirudia tena.

Waziri wa fedha nchini Marekani Timothy Geithner anatarajiwa kuwasilisha mpango wa mabadiliko ya mfumo wa uchumi wa Marekani katika bunge hii leo pamoja na kwenye kamati inayohusika na maswala ya fedha katika bunge la Marekani.

Mpango huo wa rais Obama una lengo la kuipa mamlaka benki kuu nchini Marekani, ili kusimamia masuala yote ya kifedha na kuunda mbinu ambazo zinaweza kuzuia kuwepo tena kwa vyanzo vilivyo sababisha kutokea kwa mzozo wa kiuchumi uliopo sasa.

Wadadisi wanasema kuwa mabadiliko hayo yaliyopendekezwa na rais Obama ni muhimu hasa kwa masoko yanayokabiliwa na matatizo lakini pia huenda yakawa vigumu kutekelezwa.

Akiuanzisha mpango huo jana jumatano rais Obama alisema kuwa hayo ndio mabadiliko makubwa zaidi tangu mwaka 1930, yaliyo na lengo la kuzuia kuporomoka kwa mifumo ya kifedha ambayo mara nyingi hutokana na kuwepo kwa madeni.

Hata hivyo kuna baadhi ya wanaoukosoa mpango huo wakisema kuwa, hautafanikiwa vile inayohitajika huku wengine wakisema kuwa serikali itakuwa na ushawishi mkubwa juu ya sekta za kibinafsi.

Kati ya mapendekezo kwenye mpango huo ni pamoja na kuipa benki kuu madaraka ya kuingilia kati mifumo ya uchumi ambayo inaonekana kuhatarisha uchumi ikiwemo ile ambayo haimiliki mabenki.

Hatua hizi ni muhimu na zinahitajika, lakini zinakosa mabadiliko makuu ambayo yangesaidia katika kutimiza malengo haya, alisema Douglas Elliot mwana uchumi mmoja katika taasisi moja nchini Marekani.

Mwana uchumi huyo alisema kuwa pia kunahitajiwa kufanyika mabadiliko katika makampuni makubwa, ambayo yanaweza kusababisha kuyumba kwa uchumi na pia na kuwalinda wananchi kiuchumi, matamshi ambayo pia yalitolewa na kundi linalowajumuisha wafanibiashara pamoja na wasomi lililobuniwa mwaka 2006.

Mpango huo unatajwa kulenga moja kwa moja masuala muhimu pamoja na mabadiliko makubwa na kuweka mikakati ya kukabiliana na masula yaliyochangia kutokea kwa mzozo uliopo sasa.

Hata hivo wengi wameukosoa mpango kuwa kuwa mkali, ambao huenda ukazuia uwekezaji katika mifumo ya uchumi. Wanasema kuwa mpango huo utalegeza huduma zinazotolewa na mifumo ya kuichumi na kutoa uishindani kati ya makampuni makubwa na yale ambayo bado ni madogo.

Hali kadhalika kuna wasi wasi, kwa wale wanaoutaja mpango huo kama ulio mkubwa mno, na huenda ukawa vigumu kuutekeleza na vile vile ukatoa hali ya kutokuwepo kwa utabiri katika siku za mbeleni kwenye masoko ya kifedha na katika badhii ya mifumo ya uchumi.

SHIRIKA LA AL LAONYA KUWA MATESO BADO YAPO ZIMBAMWE


Shirika la Kutetea Haki za binadamu Amnesty International limeilaumu serikali ya Zimbabwe kwa kuendelea kuhusika na vitendo vya mateso yanayokiuka haki za binadamu.Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Shirika hilo Irene Khan aliyefanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara ya siku 6 nchini Zimbabwe.

Kulingana na Bibi Khan visa vya ghasia zilizo na misingi ya kisiasa vimepungua ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita lakini bado vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinaendelea kutokea.Kauli hizo zimetolewa wakati ambapo wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na Zimbabwe wamefanya mazungumzo rasmi ya kwanza katika kipindi cha miaka 7 iliyopita.Kamishna wa masuala ya misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Ulaya Louis Michel aliyezungumza na waandishi wa habari mjini Brussels baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai alisema kuwa Umoja huo una azma ya kurejesha uhusiano kati yao baada ya kutatua baadhi ya masuala yanayozua mitazamo tofauti.

WAANDISHI WA HABARI MARUFUKU KUTANGAZA BEI ZA VIUNGO VYA ALBINO VINACHOCHEA MAUAJI YAO NCHINI TANZANIA


Na Sharon Sauwa
Washiriki wa mkutano wa kujadili mauaji ya albino, wamevitaka vyombo vya habari kutotangaza bei ya viungo vya walemavu hao.
Wamesema kufanya hivyo kunachangia kuhamasisha mauaji ya albino kwa kuwashawishi watu kufanya biashara ya namna hiyo.

Walitoa ushauri huo walipokuwa wakiwasilisha majadiliano ya vikundi jijini Dar es Salaam jana.

Hali kadhalika, wameitaka serikali kuweka wakaguzi katika maduka ya kuuza dawa za asili kama wafanyavyo katika maduka ya dawa za viwandani.

Walisema kuwa kufanya hivyo kutawawezesha kubaini iwapo dawa wanazouza haziendi kinyume na kanuni na sheria za nchi.

"Kwenye maduka haya asiyekuwa na ujuzi wa dawa za kienyeji, anauza tu ama dereva teksi anaweza naye leo hii akafungua duka la dawa za asili na anakubalika," alisema mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Rose Abdallah.

Walisema hakuna watu wanaofahamu kinachouzwa katika maduka hayo hali inayowafanya baadhi yao kuuza viungo vya wanyama wakidai kuwa vinatumika katika kuponya magonjwa mbalimbali.

ABDALLAH MOHAMED ALI (2009)


Akijaribu kupanga mikakati juu ya uongozi wake mpya mwaka 2009

HUYU NDIO MWENYEKITI MPYA WA WATANZANIA NCHINI GREECE


Si mwingine ni ndugu yetu ABDALLAH MOHAMED ALI

WATANZANIA WAISHIO MJINI ATHENS NCHINI GREECE WAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI


Kiutendaji, jumuiya hii ilikuwa ikiendelezwa na watu wachache waliokuwa na moyo na upendo wa kuona umoja wa watanzania unaendelea na kudumu. Watu hao baada ya kugundua kwamba muda muwafaka wa kufanya uchaguzi umewadia, na kwamba watu wanahitaji mabadiliko, walikubaliana kwa pamoja zitafutwe mbinu zitazohakikisha ufanikishaji wa uchaguzi.


Na hapo ndipo zilipoanza kampeni za uchaguzi, ambao ulifanyika katika ukumbi wa Sieraleone siku ya Jumamosi 07/03/2009 kuanzia saa moja usiku hadi saa tisa.Ulikuwa ni uchaguzi ULIOFANA na wa HAKI. Takriban watanzania wote walihudhuria, hata wale ambao siku za nyuma walikuwa hawana hamasa kabisa na jumuiya.Kulikuwa na kila aina ya viburudisho, vilivyosindikizwa na na mziki wa kupendeza .

Katika uchaguzi huu walichaguliwa viongozi wapya wafuatao:


MWENYEKITI
ABDALLA MOHAMED ALI. (AMASHA)

MAKAMU M/KITI
SALUM FRANCIS WILLIAM. (Mzee FRANCIS.)

KATIBU MKUU
KAYU ALLY LIGOPORA. (KAYU)

KATIBU MSAIDIZI
MUNGI HUSSEIN SALUM. ( MUNGI)
MWEKA HAZINA
AZIZI ALI. ( AZIZI )

NAIBU MWEKA HAZINA
CHINA SELEMAN HASSAN. (CHINA)

AFISA WA JAMII
ALLY MOHAMMED UBAO. ( ALI UBAO)


WAJUMBE WA KAMATI :
1 ALLY SALUM NYAU. ( ALI NYAU )
2 MWANSITI ISSA MNTAMBO. ( MWASITI )
3. MWAMVITA HATIBU MAKENGA ( MACHO )

ZE UTAMU CHINI YA ULINZI, WATANZANIA MNASEMAJE???



Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol),wamefanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani juu) mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu.Ndugu Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idara ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee Job Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.

Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania.Licha ya Ndg. Malecela Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani,ambao pia wanahusishwa na Mtandao huo wa Ze Utamu.

CHIKU NA NINDI HAWAKO NYUMA , MWANAMKE KULA!!!

AMANI KHERI AKIWA ANATAMBA KATIKA BANDA LA KWAO LA KITANZANIA

MAMBO YA MAONESHO YA SANAA MJINI ATHENS GREECE HAYO

SALAMU ZA BONGO SIKU HIZI KAMA MAMTONI TUU!!!


Mheshimiwa Ndasa..
Pichani ni Mbunge wa Sumvwe,Richard Ndasa CCM (Kushoto)akisalimiana na Mbunge
wa Chadema Lucy Owenya kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma

USHURU SASA NJEE KWA VYOMBO VYA DINI


Wiki moja baada ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kutangaza kuanza kutoza ushuru kwa mashirika yote ya Dini wakati ikiwasilisha bajeti ya Mwaka 2009/10 bungeni mjini Dodoma na kuzua maswali mengi kutoka kwa Wabunge Leo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda ametangaza Rasmi kufuta ushuru Kwa madhehebu yote ya Dini na huo na kurejea kama Mwanzo.Mheshimiwa Waziri Mkuu ametangaza Uamuzi huo Mjini Dodoma Hivi Leo

Shavu kwa Rais Jakaya Kikwete Kutoka chicago bulls

MAMBO YA KIKWETE KATIKA KIKAPU


Pichani ni jezi na mpira wenye saini za wachezaji wa timu ya Chicago Bulls ya nchini Marekani.Zawadi hizo alipewa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa ziarani Marekani hivi karibuni.Rais Jakaya Kikwete alipata kucheza mpira wa vikapu.Pichani kulia ni mwandishi wa Rais Msaidizi,Premmy Kibanga akizionyesha jezi hizo kwa waandishi wa Habari na Kushoto ni mwandishi wa Habri wa kituo cha channel 5 cha jijini Dar es Salaam BW Patric.

Thursday, June 11, 2009

TRUE LOVE EXIST





NI NDOA YA UKWELI KATI YA WAIGIZAJI WA FILAMU ZA KIBONGO AMBAPO WANAFILAMU YAO YA MBONI YANGU (SAJUKI NA WASTARA).....WALIYOIGIZA KABLA YA KUPATA AJALI ILIYOPELEKEA WASTARA KUKATWA MGUU.....HAKIKA HII INAPENDEZA NA INAONESHA UPENDO WA KWELI "UPENDO WA UJASIRI"...HONGERENI WASTARA NA SAJUKI
sherehe hiyo ilitawaliwa na vilio na majonzi, hasa pale Bibi harusi alipoingia kwenye eneo la wazi lililoandaliwa kwa shughuli hiyo akiwa amekaa kwenye baiskeli ya gurudumu (Wheel Chair).
Mke wangu sitakuacha, wewe ni mahabuba wangu, sitakuacha,” Sajuki aliimba wimbo huo. “Mume wangu unilinde, unipende, usiniache…,” Wastara naye alijibu na kusababisha vilio kutoka kwa wageni waalikwa. Aidha, yeye mwenyewe alishindwa kuendelea kuuimba wimbo huo na kujikuta akilia kwa uchungu mkubwa.
“Nimesimama hapa kwa ajili ya kumhakikishia nyonga mkalia ini wangu (Wastara) kuwa mimi ni wake milele sitomuacha mpaka kifo,” alisikika Sajuki.
Baada ya Shamrashamra hizo, Sajuki alimbeba Wastara huku akicheza naye wimbo wa mwanamuziki wa Sauzi, Yvonne Machaka ‘Chakachaka’ uitwao ‘Mkomboti’ huku akielekea naye kwenye gari kwa ajili ya kuondoka. Tukio hilo lilisindikizwa na wasanii kibao kwa nyuma huku wakicheza mpaka maharusi hao walipopanda gari na kwenda kwenye Fungate lao Kigamboni, jijini Dar es Salaam.