Wednesday, May 6, 2009

WAZIRI MKUU WA KENYA RAILA ODINGA ABATIZWA

Baadhi ya watani wetu wa jadi (Wakenya) jana walipokea ubatizo wa Waziri Mkuu Raila Odinga kwa hisia tofauti baada ya kudhihirika hakubadili jina lake, Bw Odinga alibatizwa na Askofu David Owuor wa kanisa la Holiness and Repentance Ministries mnamo jumatatu jioni, Bwana Odinga alionekana amevalia kanzu nyeupe kama ya kiislam, lakini kilichoshangaza watu wengi ni kwamba kinyume na watu wengine wanapobatizwa, Odinga ataendelea kutumia majina yake ya Raila Amolo Odinga kama kawaida.

No comments: