Saturday, May 9, 2009

JACOB ZUMA RAIS MPYA WA AFRIKA KUSINI

Capetown, Bunge la south afrika limemtangaza Jacob Zuma kuwa ni rais wa nne wa nchi hiyo. Zuma ambae ametokea kwenye chama cha ANC (African National Congress) alipata jumla ya asilimia 66 za kura zilizopigwa. Sherehe ya kutawazwa kwake imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kimataifa wapatao 30 akiwemo rais Robert Mugabe na kiongozi wa libia Muammar al Gaddaf.

No comments: