Wednesday, May 13, 2009

HAYA AMINI HUSIAMINI


Katika hara ya kushangaza watu wengiii yule mwana dada rihanna ambaye alikuwa kapewa kibano na chris brown,inasemekana kuwa ana mtindo wa kupiga picha za uchi, na sasa zimeshanyakwa na makachero, na ziko hewani kwa internate,
sasa angalia sura hii ilivyo nzuri kabla ya ugomvi na jamaa yake

USISHANGAE HII NI SURA HALISI YA RIHANNA


katika hari isiyokuwa ya kawaida rihhana alijikuta akila makofi kutoka kwa mpenzi wake chriss brown , kwa kile inachodaiwa kuwa amemuambukiza ugonjwa wa zinaa unaotokana na kujaamiana, na hapa ndio anavyoonekana baada ya kukatwa makofi,

Saturday, May 9, 2009

JACOB ZUMA RAIS MPYA WA AFRIKA KUSINI

Capetown, Bunge la south afrika limemtangaza Jacob Zuma kuwa ni rais wa nne wa nchi hiyo. Zuma ambae ametokea kwenye chama cha ANC (African National Congress) alipata jumla ya asilimia 66 za kura zilizopigwa. Sherehe ya kutawazwa kwake imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kimataifa wapatao 30 akiwemo rais Robert Mugabe na kiongozi wa libia Muammar al Gaddaf.

Wednesday, May 6, 2009

MAFURIKO YAUA 30 BRASIL


Watu 30 wamekufa na wengine 180,000 kupoteza nyumba na mali zao baada ya mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko makubwa kusini mwa nchi ya brasil. Miji isiyopungua sita imeathirika kwa mafuriko haya na watu wanakosa misaada kwa kuwa barabara zote zimesombwa na kufunikwa na maji. Serikali ya Brasil inasema itajitahidi kadri iwezavyo kuokoa wanachi wake wote kwenye janga hili.

WAZIRI MKUU WA KENYA RAILA ODINGA ABATIZWA

Baadhi ya watani wetu wa jadi (Wakenya) jana walipokea ubatizo wa Waziri Mkuu Raila Odinga kwa hisia tofauti baada ya kudhihirika hakubadili jina lake, Bw Odinga alibatizwa na Askofu David Owuor wa kanisa la Holiness and Repentance Ministries mnamo jumatatu jioni, Bwana Odinga alionekana amevalia kanzu nyeupe kama ya kiislam, lakini kilichoshangaza watu wengi ni kwamba kinyume na watu wengine wanapobatizwa, Odinga ataendelea kutumia majina yake ya Raila Amolo Odinga kama kawaida.

Tuesday, May 5, 2009

BIBI NA BWANA HARUSI WAUWAWA KWENYE SHEREHE YA HARUSI YAO

Huyu ni mmoja wa majeruhi waliojeruhiwa vibaya kwa risasi na bomu huko nchini Uturuki, baada ya watu wawili waliovaa vinyago usoni kuingia ukumbini kwenye sherehe ya harusi iliyofanyika kitongoji cha Bilge Koyu (2okm) kutoka mji wa Mardin na kufyatua risasi mfululizo na kurusha bomu na kusababisha vifo vya watu 44 wakiwemo bibi na bwana harusi siku ya jumatatu jioni . Sababu kubwa ni kwanini bibi harusi aolewe na mtu wa kabila lingine,

Friday, May 1, 2009

"Netherlands Queens Day Drama" Badala ya sherehe ni msiba








Tarehe 30 ya mwezi wa April kila mwaka ni siku ya kuzaliwa kwa malkia wa uholanzi, hii ni sikuuu kwa wananchi na wakazi wa uholanzi, Mwaka 2009 umekuwa ni siku ya wa majonzi kwa taifa la uholanzi baada ya Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Karst T. mwenye umri wa miaka 38 alipovamia umati wa watu waliokuwa wakimshangilia malkia na familia yake na kuwagonga na gari alilokuwa akiendesha na kusababisha vifo vya watu 7 na kujeruhi 14 katika mji wa Apeldoorn ambapo sherehe hiyo ilifanyika rasmi, mtuhumiwa alifariki muda mchache baada ya tukio. Mungu awapumzishe marehemu kwa amani.