Sunday, October 25, 2009
MARUBANI WASAHAU KUTUA NDEGE
Wasiwasi mkubwa uliwakumba wana anga wa kimarekani siku ya ijumaa tarehe 23 october pale ambapo ndege ya NWA ilipokosa mawasiliano kwa kipindi cha dakika 78. Ndege hiyo ambayo ilikuwa inatokea San Diego kuelekea Minneapolis na ikiwa imebeba abiria 144.
Pamoja na jitihada za kuwapigia simu na kufanya mawasiliano ya aina yote bila mafanikio iliwafanya Wana Anga wakimarekani kupeleka mawazo yao moja kwa moja kuwa ndege hiyo imetekwa nyara.
"Tulikuwa tukiwaona kwenye radar na kuwazungumzisha ila hatukupata jibu, hilo jambo lilitutia wasiwasi sana hayo" ni maneno ya msemaji mkuu wa wana anga hao mr Toni Molinari.
Imesadikiwa ya kuwa marubani hao walipitiwa na usingizi ndio maana hawakuweza sikia wala kujibu ujumbe wowote uliotumwa kwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment