Tuesday, September 15, 2009

MRUSHA VIATU MAARUFU DUNIANI AACHIWA HURU



Mwandishi wa habari ambae alimrushia kiatu rais wa zamani wa marekani bwana G.Bush ameachiwa huru leo, mwandishi huyu ambae anajulikana kwa jina la Muntazer Al Zaid amejipatia umaarufu kwa kitendo chake kinachoitwa cha ushujaa kwa kumrushia rais mstaafu huyo viatu, kwa kile alichosema ni msisitizo wa kutaka wanajeshi wa kimarekani waondoke nchini irak.
Aliachiwa huru tangu jana ila kutokana na kutotimia kwa baadhi ya fomu za kuachiwa huru ikabidi atoke leo, Anasema kuwa alipata mateso mengi sana moja wapo ni kupigwa shoti ya umeme nk. ila anafuraha kwa kuwa huru, na watu wanamuona ni shujaa.

No comments: