Showing posts with label created by mizz. Show all posts
Showing posts with label created by mizz. Show all posts

Saturday, June 20, 2009

ZE UTAMU CHINI YA ULINZI, WATANZANIA MNASEMAJE???



Polisi wa Tanzania kwa kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol),wamefanikiwa kumshika Raia mmoja wa Uingereza ambaye ana asili ya Tanzania Ndg Malecela Peter Lusinde (pichani juu) mwenye umri wa miaka 39 na kutuhumiwa kwa kuundesha mtandao wa Ze Utamu.Ndugu Malecela ambaye anajulikana pia kwa jina la "Male" ni Mtaalamu wa kompyuta na ana uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiingereza,kiswahili na kichina ana makazi katika mji wa Essex nchini Uingereza.

Wataalamu wa Idara ya upelelezi kutoka Tanzania wakishirikiana na wenzao wa Uingereza wamefanikiwa kuonana na Ndg Male na kupata ushahidi wa kutosha kwamba ndiye alikuwa mmiliki wa Mtandao huo.Idara ya Upelelezi na polisi wa Uingereza wameutaarifu Ubalozi wa Tanzania mjini London kuhusu suala hilo.Maofisa Ubalozi Mr.Clement Kiondo na Amos Msanjila wamefahamishwa jambo hilo.Malecela ni Mtoto wa Mzee Job Lusinde ambaye amewahi kufanya kazi kwenye nyadhifa mbalimbali za utumishi wa serikali Nchini Tanzania.

Habari zilizothibitishwa zinadai kuwa Ndg Malecela amerudishwa Tanzania kwenda kujibu tuhuma mbalimbali za kuendesha mtandao uliokuwa unadhalilisha watu,kuna malalamiko 6850 yaliyoandikishwa kulaumu udhalilishwaji wa watu uliofanywa na mtandao huo,Mtandao huo ulisimamishwa mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa maombi ya serikali ya Tanzania baada ya kutoa picha ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,ufuatiliaji uliofanywa baada ya picha hiyo ndio umepelekea kukamatwa kwa Ndg Malecela.

Haijaeleweka wazi Ndg Malecela atashitakiwa kwa sheria gani? Lakini ni wazi kwamba atashitakiwa Nchini Tanzania.Licha ya Ndg. Malecela Polisi wa Upelelezi wamezungumza na Watanzania wengine wawili katika miji ya Wichita na San Diego Nchini Marekani,ambao pia wanahusishwa na Mtandao huo wa Ze Utamu.

Saturday, April 11, 2009

OBAMA KATIKA MAISHA YAKE KABLA YA URAISI JE UNAYAJUA?





























Hahaha, haya ndio maisha aliyokuwa nayo rais wa marekani wa sasa Barack Hussein Obama, haya jamani angalieni wenyewe

Tuesday, April 7, 2009

RAMANI MPYA YA JIJI LA DAR ES SALAAM


Hii ndio ramani mpya ya jiji la dar es salaam tanzania, ambayo inatarajiwa kuanzwa kushugulikiwa haraka iwezekanavyo baada ya pesa za epa kurejeshwa zote, Imekuwa ni ndoto ya kila mtanzania kutaka kuona mji mpya wa dar es salaam ukijengwa upya na kuwa wa kisasa kama ramani yake inavyoonekana juu pichani,

Monday, April 6, 2009

TETEMEKO LA ARDHI LAUA WATU ITALY







Katika hali isiyo tegemewa nchini italy yametokea maafa makubwa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 270, watu wengine zaidi ya kumi elfu kukosa mahali pa kushi na zaidi ya 1500 wakiwa majeruhi, tukio hilo lilitokea alfajiri ya mapema ya jumanne tarehe 7 april huko mjini L'Aquila.




Saturday, April 4, 2009

Haya maisha bado ni kawaida kwa mtanzania


Huwezi amini katika maisha ya mtanzania bado ni kitendawili katika swala zima la sekta ya miundombinu, siku mvua inaponyesha basi inakuwa ni kama kiyama kwa mtanzania , bara bara zinafurika , foleni haziishi, na hata maji taka hayana pa kwenda, je lini tutafika jamani namna hii.